Makamu wa Rais, Dkt. Philip Mpango amewataka wananchi wa Wilaya ya Buhigwe kufanya kazi kwa bidii ikiwa ni pamoja na kutumia vema fursa za miradi iliopo wilayani humo kujipatia maendeleo.

Dkt. Mpango ameyasema hayo mara baada ya kukagua ujenzi wa shule mpya ya sekondari ya wasichana kidato cha tano na sita, yenye jumla ya majengo 18 inayojengwa katika kata ya kajana Kijiji cha kasumo.

Jengo la shule mpya ya sekondari ya wasichana kidato cha tano na sita yenye jumla ya majengo 18 inayojengwa katika kata ya Kajana kijiji cha Kasumo wilayani Buhigwe Mkoani Kigoma.

Akiwa eneo hilo, Dkt. Mpango pia amekagua ujenzi wa jengo la Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), wilaya ya Buhigwe, Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Buhigwe na Ujenzi wa Nyumba ya Mkuu wa Wilaya.

Aidha, Makamu wa Rais pia amewasihi wakandarasi kuendelea kutoa fursa ya kazi kwa wazawa wa maeneo husika ya ujenzi, ili waweze kujiinua kiuchumi.

Wabunge wa Odinga kortini kwa uvunjifu wa sheria
Mabadiliko DRC: Tshisekedi awateua Bemba, Vital Khamere