Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ametembelea katika maonyesho ya Maadhimisho ya Siku ya Kifua Kikuu Duniani, yaliyofanyika Kitaifa  kwenye uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu.

Majaliwa ametembelea maonesho hayo hii leo Machi 24, 2023 na akiwa katika viwanja hivyo alipata maelezo kutoka kwa Mwalimu wa panya wanaonusa na kubaini mate au makohozi yenye vijidudu vya ugonjwa wa Kifua Kikuu.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Mwalimu wa panya wanaonusa na kubaini mate au makohozi yenye vijidudu vya ugonjwa wa Kifua Kikuu, Mariam Chamkwata wa Chuo Kikuu cha Kilimo, Sokoine cha Morogoro.

Mwalimu huyo, ni Mariam Chamkwata wa Chuo Kikuu cha Kilimo, Sokoine cha Morogoro, ambaye alikuwa kitoa maelekezo kwa Waziri Mkuu ambaye aliambatana na Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu na viongozi wengine wa Mkoa.

Akiwa eneo hilo, pia Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alisalimiana na Viongozi mara baada ya kuwasili kwenye viwanja hivyo vya Halmashauri ya Mji wa Bariadi kuwa mgeni rasmi katika Maadhimisho hayo ya Siku ya Kifua Kikuu Duniani.

Mabadiliko DRC: Tshisekedi awateua Bemba, Vital Khamere
Mwamba anarudi Singida Big Stars 2023/24