Uongozi wa klabu ya Singida Big Stars umemuongezea muda wa likizo nyota wake Dario Frederico, ambaye alikuwa amepewa likizo ya mwezi mmoja kwa ajili ya matibabu nchini Brazil na hivi sasa ripoti ya daktari imeonesha kuwa amepona kwa zaidi ya 90%.

Hivyo klabu hiyo imemuongezea muda zaidi ili aweze kuwa timamu kwa 100% apate na muda wa kutosha wa kupumzika.

Hivyo kutokana na kuongezewa muda wa likizo klabu imeeleza kuwa Frederico atarejea na kujiunga na kikosi hicho wakati wa maandalizi ya ligi kuu msimu ujao (Pre-season) 2023/24 huko nchini Tunisia.

Wakati akiondoka nchini mwaka 2022, Dario alikiri kuondoka kuwa na ruhusa maalumu ya viongozi na kueleza hakuna mgogoro baina yake na waajiri wake kama inavyoelezwa baada ya kuondoka kwake.

“Sina mgogoro wowote na viongozi wangu, hivyo nipende kuwahakikishia mashabiki na wachezaji wenzangu nipo kwa ajili ya kuipigania timu na muda siyo mrefu tutajumuika tena pamoja kuendeleza harakati zetu,” alisema.

Dario Frederico alikuwa mchezaji watatu kuondoka Singida Big Stars akitanguliwa na mwenzake, Peterson Cruz na Muargentina, Miguel Escobar ingawaje wawili hao hawakuweza kurudi tena nchini kwani walipata timu nyingine.

Dario Frederico alisema alirejea Brazil kwa ajili ya mambo ya kifamilia huku akiwatoa hofu mashabiki zake atarejea muda sio mrefu kuendelea na majukumu kama kawaida.

Panya atumika kubaini vijidudu ugonjwa Kifua Kikuu
Nape awakubali waleta mageuzi sekta ya Mawasiliano