Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye amesema Serikali itaendelea kuunga mkono jitihada zinazofanywa na wawekezaji katika sekta ya mawasiliano ambao wanaleta mageuzi.

Waziri Nape amesema hayo jijini Dar es Salaam wakati alipotembelea kituo cha mkongo wa mawasiliano cha 2 Afrika kinachosimamiwa na Kampuni ya Airtel ambacho kikikamilika kitawezesha kuziunganisha nchi zaidi ya 30 Barani Afrika.

Amesema, “Kwanza niwapongeze Airtel kwa kuliona hili ambalo litaleta mageuzi makubwa kwenye sekta ya Mawasiliano, mkongo huu utakuwa wenye kasi zaidi na utasaidia kuunganisha watu kwa mataifa tofauti, hivyo naamini utatatua kwa kiwango kikubwa changamoto za kimawasiliano.”

Aidha, Nape amesema kuongezeka kwa mkongo uliopita chini ya Bahari ni dalili nzuri kwani watoa huduma, watakaokuwa na nafasi ya kufanya machaguo juu ya mkongo upi utumike na kuweza kuchangia kushuka kwa gharama na ongezeko la ubora wa huduma za Intaneti.

Mwamba anarudi Singida Big Stars 2023/24
Wachezaji Zanzibar wapigwa marufuku Ndondo Cup