Shirikisho la soka Barani Afrika CAF limeupiga chini Uwanja wa CCM Kirumba kutumika kwa ajili ya michuano ya Kimataifa msimu wa 2021/22.
Uwanja wa CCM Kirumba ulitarajiwa kutumiwa na timu ya Biashara United Mara kwa ajili ya michezo ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika itakayoanza baadae mwezi huu.
Meneja na mratibu wa Biashara United Mara amesema wamepokea taarifa za kukataliwa kwa Uwanja huo, hivyo wamelazimika kubadili kila kitu, kwani walikuwa Kirumba kwa zaidi ya siku 10 na wachezaji walikuwa wamezoea mazingira.
Biashara United Mara itaanzia nyumbani kwa kucheza dhidi ya FC Dikhil ya Djibouti, na ni rasmi sasa mpambano huo utapigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa.