Kikosi cha cha wachezaji 24 na viongozi 6 cha Maafande wa Jeshi la Polisi (Polisi Tanzania FC) kinatarajia kuweka kambi jijini Mwanza, tayari kwa maandalizi ya Msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2021/22.

Polisi Tanzania FC imepanga kufanya mazoezi kwa siku kadhaa sambamba na kucheza michezo ya Kirafiki dhidi ya timu za Kanda ya Ziwa, ambayo wanaamini itawaweka sawa kabla ya kuanza kwa Mshike Mshike wa Ligi Kuu Tanzania Bara utakaoanza Septemba 29.

Taarifa iliyotolewa na Uongozi wa klabu hiyo imeeleza kuwa wachezaji wengine watano watajiunga na timu ikiwa Mwanza, baada ya kumaliza majukumu yanayowakabili kwa sasa.

Wachezaji hao ni Mohmmed Mmanga, Juma Ramadhani, Daruweshi Saliboko na Mlinda Lango Metacha Boniface Mnata aliyejiunga na Maafande hao akitokea Young Africans.

Watanzania kuchezesha URA vs Coffee SC
Uwanja wa CCM Kirumba wakataliwa CAF