Shambulio lililotajwa kuwa ni latano la aina yake Ansarullah dhidi ya Saudi Arabia katika wiki za hivi karibuni limethibitishwa kufanyika na kundi la Ansarullah nchini Yemen.
Kundi hilo limetangaza kuwa limeshambulia uwanja wa ndege wa Jazan kusini Magharibi mwa Saudi Arabia kwa kutumia ndege zisizo na rubani.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na jeshi la anga la Yemen limesema kuwa mashambulizi hayo yamelenga uwanja na maegesho ya ndege zisizo na rubani zinazotumiwa na Saudi Arabia dhidi ya taifa la Yemen.
Wapiganaji wa Ansarullah wamezidisha mashambulizi yao dhidi ya Saudia katika wiki za hivi karibuni na jumatano iliyopita waliteka vituo 20 vya jeshi la nchi hiyo katika eneo la Najran huko kusini mwa Saudia.
Ikumbukwe kuwa wiki tatu nyuma, ndege zisizo na rubani za Ansarullah zilifanya mashambulizi manne ambayo yalilenga mfumo wa kujikinga na makombora wa Patriot na kambi ya kijeshi ya eneo la Najran.
Makamanda wa harakati ya Ansarulla wamesema kuwa mashambulizi hayo ni jibu la jinai na mauaji yanayoendelea kufanywa na watawala wa Saudi Arabia na waitifaki wao dhidi ya raia wasio na hatia wa Yemen.