Mwenge wa Uhuru kitaifa 2023, umeweka jiwe la Msingi katika mradi wa Maji wa Nzuguni Jijini Dodoma ambao utaongeza hali ya uzalishaji wa maji kutoka lita milioni 68.6 hadi lita milioni 76 sawa na ongezeko la asilimia 11 kwa Siku.

Akisoma taarifa ya Mradi huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira -DUWASA, Mhandisi Aron Joseph amesema lengo la Mradi huo ni kuboresha huduma ya maji kwa kuongeza hali ya uzalishaji maji Jijini Dodoma.

Amesema “hadi sasa Mradi huo umefika Asilimia 85 za Utekelezaji wake ambapo Mamlaka hiyo inatekeleza Mradi huo kupitia Wazabuni wa Saba Mradi huo mkubwa unaotekelezwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira (DUWASA) unagharimu Sh4.8 bilioni na unategemewa kuongeza asilimia 11 ya upatikanaji wa maji katika Jiji la Dodoma kwa kuwanufaisha wakazi 75,968.”

Hata hivyo, amesema Jiji la Dodoma linazalisha nusu ya mahitaji ya maji ambapo mahitaji ya maji ni lita milioni 133 kwa siku na yanayozalishwa ni lita milioni 67.8 hivyo kuwa na upungufu wa lita milioni 66.7 kwa siku.

Naye Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini na Waziri wa Madini, Anthony Mavunde amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa namna alivyoweza kuwatatulia changamoto ya Maji hasa katika kata ya Nzuguni Jijini humo.

Ushawishi wa Messi umetiki Marekani
Serikali yawarudisha Wazazi kwenye malezi