Baada ya kuibuka taarifa kwamba Lionel Messi amewaomba mabosi wa Inter Miami wamsajili kiungo wa Real Madrid na timu ya taifa ya Coatia, Luka Modric  inaelezwa kuwa vigogo hao tayari wameshaanza mazungunzo kwa ajili ya kumsajili kiungo huyo kupitia dirisha lijalo.

Modric ambaye katika dirisha lililopita alikataa kutimkia Saudi Arabia licha ya kupokea ofa nono, mkataba wake na Real Madrid utafikia kikomo mwishoni mwa msimu huu 2023/24.

Hata hivyo, ili kuipata huduma ya mchezaji huyu Inter Miami itatakiwa kuweka ofa nono kwani matajiri wa Saudia bado hawajakata tamaa kwenye mchakato kutaka kumsajili.

Modric ambaye amewahi kunukuliwa kwamba bado anatamani kucheza soka la ushindani, kuna uwezekano mkubwa pia akarudi Croatia ambako timu yake ya utotoni ya Dinamo Zagreb imeonyesha nia ya kutaka kumsajili ili akamalizie soka lake huko.

Messi ni mmoja kati ya mashabiki wakubwa wa kiungo huyu na anaamini akitua Inter Miami, atakwenda kuongeza ubora katika eneo la kiungo na ushambuliaji.

Wamerejea kuikabili Tanzania Prisons
Uzalishaji wa maji kufikia lita milioni 76 Nzuguni