Maafisa wa afya nchini Thailand wametoa masharti kadhaa kwa wapendanao na siku ya wapendanao hasa katika kushiriki tendo la ndoa ili kuzuia kuenea kwa visa vya UVIKO 19 ambavyo vinaendelea kuongezeka.
Maafisa hao wamesema ni vyema kuvaa maski wakati wa kushiriki tendo la ndoa ili kuwazuia wapenzi kubusiana kukiwa na ongezeko la visa vya UVIKO 19 nchini ambavyo serikali inahofia huenda vikaongezeka Jumatatu, Februari 14.
Kulingana na ripoti ya Daily Mail, maafisa hao walibaini kuwa ingawa UVIKO 19 sio ugonjwa wa zinaa, unaweza kuenea kwa kugusana na kubusiana hivyo ni vyema kuvalia maski ili kuwazuia wapenzi kubusiana na kuzuia kugusana ili kujilinda dhidi ya COVID-19.
Pia wapenzi walishauriwa kupimwa virusi vya corona kabla ya kushiriki matendo ya kuoneshana mapenzi siku ya wapendao.
“Ikiwezekana, kuvaa barakoa wakati wa kufanya ngono kunaweza kusaidia kupunguza hatari za COVID-19,” mkurugenzi wa Ofisi ya Afya ya Uzazi Bunyarit Sukrat alisema.
Siku ya Wapendanao ni siku maalum nchini Thailand na wanandoa mara nyingi huchagua siku hii kuwa siku yao ya harusi.