Waziri wa Katiba na Sheria, George Simbachawene amewataka vijana wasomi kuwa wazalendo kujenga uchumi na kuwa na ajenda ya pamoja ya kukabiliana na kero mbalimbali ikiwamo ajira.

Simbachawene amesema hayo leo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari  kuhusu maombi ya Kitaifa yaliyoandaliwa na Taasisi ya Kingdom Leadership Network iliyoshirikisha vijana mbalimbali nchini lengo kuwapa elimu ya masuala muhimu ya kujiinua kiuchumi.

Amesema tatizo la ajira hivi sasa lipo ulimwenguni kote na kuwataka kuchangamkia fursa zilizo halali za kujikwamua kiuchumi.

“Sasa hivi kumekuwa na vijana wasomi wengi na wengine bado hawana ajira lakini naamini kupitia makongamano haya ni fursa zakuweza kuwatoa walipo na kujiajiri wenyewe badala yakutegemea kuajiriwa,”amesisitiza

Bwalya, Chama, Kanoute, Morrison wana kazi maalum Simba SC
Vaeni barakoa wakati wa kushiriki mapenzi