Kocha Mkuu wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC Sven Vandenbroeck, amesema ana uhakika kikosi chake kitafanya vizuri katika mchezo wa mzunguuko watatu wa Ligi Kuu dhidi ya Biashara United Mara, utakaochezwa mwishoni mwa juma hili jijini Dar es salaam.
Simba wameshashuka dimbani mara mbili tangu Msimu huu ulipoanza Septemba 06, huku wakiambulia alama nne zilizotokana na ushindi wa mabao mawili kwa moja dhidi ya Ihefu FC na kisha sare ya bao moja kwa moja dhidi ya Mtibwa Sugar.
Kocha huyo amesema uhakika wa kufanya vizuri katika mchezo wa mzunguuko watatu dhidi ya Biashara United Mara, anaupata kutokana na utayari na umahiri wa wachezaji wake, licha ya kukabiliwa na changamoto kwenye mchezo uliopita dhidi ya Mtibwa Sugar.
“Michezo ya kwanza huwa ngumu na isiyotabirika, ila safari ya kutetea ubingwa iko pale pale na tutaianza vema katika mchezo wetu wa unayofuata, kwa sasa ni mapema kusema lolote maana ndio kwanza Ligi Kuu imeanza, huku pia tukijipanga na michuano ya kimataifa,” amesema kocha Sven.
Hata hivyo kocha huyo kutoka nchini Ubelgiji amesema anafurahishwa na viwango vya wachezaji wake, kwani tangu wlipoanz asafari ya kutete taji msimu huu hawajacheza vibaya, licha ya kuambulia alama nne kwenye michezo miwiwli.
Kikosi cha Simba kimesharejea jijini Dar es salaam, kikitokea Morogoro, na kitaanza maandalizi ya kuelekea pambano dhidi ya Biashara United Mara, litakalopigwa Uwnaja wa Benjamin Mkapa, Jijini Dar es salaam.