Beki kutoka nchini Ufaransa Lucas Hernandez, ameweka wazi mpango wake wa kuendelea kuwatumikia mabingwa wa Ujerumani FC Bayern Munich, kulingana na mkataba wake klabuni hapo.

Beki huyo wa pembeni ambaye alikua sehemu ya kikosi cha Ufaransa kilichotwaa ubingwa wa Dunia 2018, bado ana mkataba wa miaka minne na FC Bayern Munich, ambayo ilimsajili akitokea Atletico Madrid kwa kitita cha 80 msimu 2019-20.

Mabingwa wa soka nchini Ufaransa Paris Sanit-Germain wamekuwa wakihusishwa na mpango wa kutaka kumsajili, katika kipindi hiki cha usajili wa majira ya kiangazi.

Hata hivyo Hernandez amepanga kuendelea kusalia FC Bayern Munich ambao msimu uliopita walitwaa mataji ya Bundesliga, DFB-Pokal na Ligi ya Mabingwa Ulaya wakiwa chini ya meneja Hans-Dieter Flick.

“Kuondoka Bayern? Hapana, bado nina miaka minne kwenye mkataba wangu niliyo saini,” amesema Hernandez.

“Lakini itategemea na msimu huu kama sintofahamu ya kupata nafasi ya kucheza itaendelea tutanagalia nini kitafuata.”

Hernandez amekuwa akisumbuliwa na majeraha ya kifundo cha mguu aliyopata mwezi Oktoba mwaka jana, na amekuwa akipambana kupata muda zaidi wa kucheza huku nafasi anayocheza kukiwa na David Alaba na Alphonso Davies.

Vandenbroeck atuma salamu Biashara Utd Mara
Suga njia nyeupe kuwa Waziri Mkuu - Japan