Staa wa muziki hapa nchini, Vanessa mdee anye peperusha vyema bendera ya Tanzania katika muziki wa Bongo fleva anakuja na show yake mpya iitwayo ”Deep Dive with Vanessa Mdee” amabyo iitakuwa kwa mfumo wa PodCast inatarajiwa kuanza kesho Januari 7.
Kupitia show hiyo msanii huyo ameeleza kuwa ndani yake kutakuwa na mengi ya kujifunza amabpo atakuwa akiongelea kuhusu jamii inayomzunguka na maisha yake binafsi
Hata hivyo msanii huyo kwasasa ameachia kionjo cha show yake hiyo iliyopo kwenye Youtube channel yake ambapo ameonglea mengi ambayo mashabiki zake hawayajui.
Aidha PodCast ni aina ya Show ambayo uwasilishwaji wake ni kwa njia ya mfumo wa Sauti bila picha wala video ni Sauti tu.