Venezuela imemfukuza nchini mwake balozi wa Ujerumani, Daniel Kriener hatua ambayo imekosolewa vikali na mataifa yanayomuunga mkono kiongozi wa upinzani, Juan Guaido huku Marekani ikitangaza vikwazo zaidi Venezuela.

Wizara ya Mambo ya Nje imempa balozi huyo wa Ujerumani masaa ya 48 ya kuondoka nchini humo kwa madai ya kuingilia masuala ya ndani ya Venezuela, huku balozi huyo alionekana katika uwanja wa ndege wa Caracas akimkaribisha Juan Guaido wakati alipokuwa akirejea nchini humo siku ya Jumatatu.

Aidha, Guaido amesema kuwa, hatua ya kufukuzwa kwa Kriemer itachukuliwa kama kitisho dhidi ya ulimwengu ambapo alikuwa miongoni mwa mabalozi wengine waliomkaribisha, Guaido anayetambuliwa na mataifa zaidi ya 50 kama rais wa mpito.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani, Heiko Maas amesema kuwa hatua hiyo inayotajwa na wachambuzi wa Venezuela kama ujumbe kwa walio mstari wa mbele kuipinga serikali ya Maduro inazidi kudhoofisha hali ya mambo.

Kwa upande wake Makamu wa rais wa Marekani, Mike Pence amesema kuwa serikali yake imeiongezea vikwazo vingine nchi hiyo ili kumshinikiza Maduro kuondoka madarakani kwa kufuta vibali 77 vya kusafiria kwa watu wenye mahusiano na Maduro.

“Ninawaahidi Wamarekani wenzangu tutaendelea kuwa imara. Na hii leo wizara ya mambo ya nje inatangaza kuwafutia vibali vya kusafiria raia 77, wakiwemo maafisa wa serikali ya Maduro na familia zao, tutaendelea kuiwajibisha serikali ya Maduro hadi pale taifa hilo litakapokombolewa,”amesema Pence

 

Rais Kagame amaliza ziara yake hapa nchini
Video: Aliyosema Kibonde kuashiria kifo chake, Kamwene Mbowe na Matiko