Rais wa Klabu Bingwa nchini Italia SSC Napoli, Aurelio de Laurentiis, amebainisha kwamba, wameingia kwenye makubaliano na Mshambulaiji wao kutoka NIgeria Victor Osimhen wa kuongeza mkataba mpya.

SSC Napoli inataka kumuongezea Osimhen mkataba wa miaka miwili katika mkataba wake wa sasa, na kuvunja tetesi zote zinazomuandama Mshambuliaji huyo ambaye anawindwa na klabu za England na Ujerumani.

Mshambuliaji huyo kutokana na uwezo wake mzuri wa kufunga mabao, amekuwa akiwindwa na timu nyingi Ulaya ikiwemo Manchester United, Chelsea na Bayern Munich, huku dau lake la Pauni Milioni 150 likiwa kikwazo kuuzwa.

Katika msimu wa 2022-23, Osimhen alitisha kunako Ligi Kuu ya Italia maarufu Serie A akiibuka mfungaji bora akifunga mabao 26.

“Tupo kwenye makubaliano na Victor Osimhen kwa ajili ya kuongeza miaka miwili katika mkataba wake.

“Kama kuna timu itatokea kwa ajili ya kutaka kumsajili tutaangalia na kufanya maamuzi ambayo yatakuwa na faida kwa klabu,” amesema rais huyo.

Punda wasababisha maandamano Kenya
Fiston Mayele awajibu waliombeza 2022/23