Mfalme wa Bongo Fleva mwenye sauti ya dhahabu, Ali King Kiba, jana ameachia ngoma yake kali sana na kuitambulisha kama ngoma isiyo rasmi, na amesema kuwa amefanya hivyo kuwafurahisha mashabiki wake katika siku yake ya kuzaliwa.
Ali King Kiba amefanya ngoma hiyo kwa ustadi mkubwa hasa katika upande wa video hii ni moja kati ya ngoma kali alizowahi kufanya na kutendea haki upande wa Video.
Tazama vedio: Ali Kiba ”Maumivu Perday”
Ali Kiba amekuwa na historia ya kufanya audio kali na kuvuruga upande wa video, hilo mashabiki wake wamekuwa wakilalama sana.
Lakini kupitia maoni hayo kutoka kwa mashabiki wake Ali sasa anawekeza sana katika video anatengeneza nyimbo kali na video kali zinazokubadilika na jamii yote.
King amewahi kufanya ngoma moja kali iliyoenda kwa jina a chekecha, ni ngoma iliyofanya vizuri sana upande wa audio na kuwatengenezea mashabiki wake kuwa na matarajio makubwa upande wa video, matarajio hayo yaliyeyuka mara baada ya video hiyo kuachiwa rasmi.
Hata hivyo wasanii wengi siku hizi wanawekeza kwenye video, wanafanya mziki mbaya lakini matayarisho ya video hiyo yanakuwa makubwa sana, nahii yote ni kutokna na ukuaji wa teknolojia na utandawazi.