Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo amesema kuwa kuna haja kubwa ya kuyafanyia uchanguzi makanisa ili kuweza kujua makanisa halisi ili kuweza kutofatisha na mawakala wa shetani.
Ameyasema hayo jijini Arusha ambapo amesema kuwa baadhi ya makanisa yamekuwa yakiwapotosha wananchi kwa kuwajaza imani isiyokuwa ya kibinadamu.
Amesema kuwa historia ya mchungaji Kakobe inatia mashaka kwani amebeba vyeo vyote vya kanisa hata anaposafiri huwawekea waumini wake ‘Cassete’ ili wamsikilize akiwa safarini.
“Kuna watu wengine ni mawakala wa shetani, hivyo kuna kila haja ya kuanza kufanya uchambuzi wa makanisa haya ambayo yamekuwa yakipotosha Watanzania, unaofanywa na anayejiita Askofu Kakobe ni umburula,”amesema Gambo
Hata hivyo, ameongeza kuwa taasisi ya dini ina utaratibu wake inaheshimika, ina mfumo wake na inathaminika katika jamii.