Oktoba 17, 2019 Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HELSB), Abdul-Razaq Badru ametangaza orodha ya awamu ya kwanza yenye wanafunzi 30,675 wa mwaka wa kwanza kwa mwaka wa masomo 2019-2020 waliofanikiwa kupata mikopo yenye thamani Tsh. 113.5 bilioni, katika orodha hiyo, wanaume ni 19,632 (64%) na wanawake ni 11,043 (36%).
