Msanii wa muziki nchini aliyekuwa anafanyia kazi zake chini ya Lebo ya WCB, ambaye siku kadhaa zilizopita alijiengua kufanya kazi chini ya lebo hiyo na kuanzisha lebo yake inayoenda kwa jina la Konde Gang, Harmonize huenda mwaka huu akashiriki tamasha kubwa la muziki la Fiesta 2019.

Hayo yamekuja mara baada ya Harmonize kuonekana kuwa karibu na mmoja wa wanafamilia wa Clouds ambaye pia ni muandaaji mkubwa wa Tamasha hilo.

Aidha, imetangazwa kuwa hivi karibuni Harmonize ataweka wazi menijimenti itakayokuwa inasimamia kazi zake za muziki ndani na nje ya Tanzania.

Sikiliza Video hapa Chini.

Mmiliki wa Facebook aweka msimamo kuhusu zuio la siasa
Video: Bodi ya mikopo yataja majina ya wanafunzi watakaonufaika na mkopo 2019/20