Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimesema kuwa kitaendelea kusaidiana Chama cha Wananchi (CUF) upande wa Maalim Seif Sharifu Hamad katika kuhakikisha kuwa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) inaendelea kuwa nguvu.
Hayo yamesemwa na Waziri Mkuu Mstaafu na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Fredrick Sumaye alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam, ambapo amesema kuwa Chadema itaendelea kumuunga mkono Maalim Seif.
“Chadema tutaendelea kumuunga mkono na kushirikana na Chama cha Wananchi CUF ya upande wa Maalim ili kuepusha kuzoofika kwa umoja wetu ambao umekuwa na nguvu kubwa, kama tukimuacha peke yake basi tutakuwa tumepungukiwa na kitu fulani,”amesema Sumaye.
Hata hivyo, Sumaye ameongeza kuwa mgogoro unaoendelea ndani ya Chama cha Wananchi CUF umetengenezwa kwaajili ya kukipunguzia nguvu chama hicho hasa kwa upande wa Zanzibar