Jeshi la polisi Mkoani Rukwa limekamata maboksi mawili yenye vito vinavyosadikiwa kuwa ni vya thamani pamoja na mchanga mweusi kutoka kwa raia wa nchi ya jirani ya Kongo kwa kisingizio cha kuleta Tanzania kwa ajili ya maonesho.

Akithibitisha hayo Kamanda wa polisi Mkoa wa Rukwa, SSP George Kyando amesema jeshi la Polisi likiwa kwenye dolia ya pamoja na Askari wa Uhamiaji walifanikiwa kukamata raia wawili wa Congo wakiwa na maboksi hayo yenye vipande vya mawe na mchanga mweuzi (nusu kilo) ambapo raia hao wa Congo wamesema kuwa mawe hayo ni yakisanii. Tazama hapa video

Rais Magufuli awapandisha vyeo na kuwateua maafisa wawili wa zimamoto
Video: Chadema wathibitisha kuungana na Maalim Seif