Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Dkt. John Pombe magufuli amewapandisha vyeo na kuwateua Maafisa wawili wa Jeshi la Zimamoto kuwa Makamishna.

Akitoa taarifa hiyo, Katibu Mkuu wa wizara ya mambo ya ndani ya nchi, Meja Jenerali Mstaafu Projesti Rwegasira amesema waliopandishwa vyeo ni Kamishna Bill Jimmy Mwakatage ambaye ameteuliwa kuwa Kamishna wa Divisheni ya Operesheni.

Kabla ya uteuzi huo, Kamishna Billy Mwakatage alikuwa Mkuu wa Rasilimali watu katika Divisheni ya Utawala wa Fedha.

Mwingine aliyeteuliwa ni Kamishna Msaidizi Jesuald Ikonko, Kamanda wa Zimamoto ambaye amepandishwa cheo na kuteuliwa kuwa Kamishna wa Divisheni ya Usalama wa Moto.

Katibu Mkuu huyo amesema kuwa Makamishna hao waliopandishwa vyeo wataapishwa na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Agosti 3, 2017 kwenye ukumbi wa mikutano wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

 

Serikali yaongeza masaa ya mama kunyonyesha
Video: Jeshi la Polisi Rukwa lakamata vito vya thamani vilivyopitishwa kimagendo