Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (Costech) imesema kuwa itayapitia machapisho ya tafiti mbalimbali zilizofanywa duniani na kuziweka kwenye mfumo wa kidijitali.

Hayo yamesemwa jijini Dar es salaam na Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Amos Nungu katika warsha iliyowakutanisha watafiti, wakutubi na wataalamu wa Teknolojia ya Habari na Mawsiliano (TEHAMA) ambapo amesema kuwa mradi  huo wa miaka mitatu unafanywa na umoja wa mataifa.

“Wenzetu kwenye nchi zilizoendelea hata maktaba zao ziko kwenye mfumo wa kidijitali, na sisi imefikia hatua tuanze kutumia hazina ya teknolojia ili kuweza kuzifikia tafiti mbalimbali zilizofanyika,”amesema Nungu

 

Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Agosti 29, 2018
Video: Lugola awachimba mkwara MaDC wanao waweka ndani wananchi