Katika kuhakikisha wizi wa mtandaoni unadhibitiwa na kukomeshwa kabisa na kuunga mkono jitihada za serikali ya awamu ya Tano yenye kauli mbiu ya “Hapa kazi tu,”

Kampuni ya Data Vision International iliyopo Mikocheni Jijini Dar es salaam, imekuja na mfumo mpya katika kuhakikisha inadhibiti wizi wa mitandaoni ambao utashirikisha mabenki yote yaliyojiunga na Umoja Switch hapa nchini.

Aidha, Data Vision International imejipanga kuanza na Mkoa wa Dar es salaam kwa kuwakutanisha wadau  wa mitandao na mabenki yaliyojiunga na Umoja Switch kwa ajili ya kuanza kufundisha mfumo huo jinsi utakavyokuwa unafanya kazi.

Hayo yamesemwa na Prof. Fredrick Mtenzi alipokuwa akiwasilisha mada katika Kongamano lililoandaliwa na Data Vision kwa kushirikiana na Umoja Switch ambalo limefanyika Zanzibar mwishoni mwa wiki.

Amesema kuwa Data Vision International imejipanga kusaidia taasisi zote za fedha za Serikali na binafsi ambazo zinafanya kazi na Umoja Switch ili ziweze kudhibiti wizi ambao siku zote umekuwa ni tatizo kubwa katika taasisi za kifedha.

Aidha, amesema kuwa Data Vision itatengeneza mfumo ambao utakuwa unakusanya taarifa zote za benki na kuzituma sehemu husika kwa ajili ya kutoa taarifa za wizi uliotokea.

Prof. Mtenzi amesema kuwa mfumo huo utasaidia kupambana na kudhibiti wizi huo unao ongezeka kadri teknolojia inavyozidi kukua.

 

 

 

Video: Meya atoa neno shule 6 zilizofanya vibaya matokeo kidato cha nne Dar
Serikali kuboresha fursa ajira za vijana nchini