Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Jenista Mhagama amesema kuwa Serikali imejipanga kusaidia vijana kutambua na kuchangamkia fursa mbalimbali za ajira zilizopo nchini ili kutatua changamoto ya ukosefu wa ajira na  kutimiza adhma ya kuleta maendeleo hususani kwa vijana.

Mhagama ameyasema hayo wakati akijibu hoja ya Mbunge wa Kinondoni Maulid Mtulia, iliyohoji juu ya jitihada za Serikali katika kutatua tatizo la ukosefu wa ajira kwa vijana wakati wa Mkutano wa Tano wa Bunge unaoendelea Mkoani Dodoma.

Katika Mkutano huo  Waziri amesisitiza kuwa Serikali ina mipango na mikakati madhubuti inayokusudiwa yakusaidia vijana wa Kitanzania ili kujiletea maendeleo yao wenyewe na kuondokana na umasikini.

“Serikali ya Awamu ya Tano imeendelea kuweka mikakati ikiwemo uwanzishwaji wa programu mbalimbali zitakazo saidia kutatua changamoto ya ajira kwa vijana kwa kuangalia matokeo ya tafiti mbalimbali ambazo zimepelekea kuwa na programu zinazolenga kukabili tatizo la ukosefu wa ajira kwa vijana” amesema Mhagama.

Amesema Pamoja na juhudi hizo zinazotarajiwa kuzaa matunda bado Waziri amewatoa hofu wananchi wote kwa kuwepo kwa fursa hizo za ajira zitakazo jali hali za watu pasipo kuangalia makabila yao, rangi wala dini.

Hata hivyo, ameongeza kuwa, Serikali pia inajitihada za kuvutia uwekezaji kwenye sekta mbalimbali na urasimishaji wa sekta isiyo rasmi ili kupunguza kiwango cha ukosefu wa ajira.

 

Video: Data Vision International kudhibiti wizi mtandaoni
Mfuko wa maendeleo ya vijana watoa mikopo kwa vikundi 309