Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mjini, Fabian Daqaro amewataka madereva wa wilaya hiyo kuendelea kuwaelimisha madereva wenzao kupitia mikutano mbalimbali ili kuweza kuepuka ajali.
Ameyasema hayo jijini Arusha alipokuwa akizungumza na madereva hao jijini humo ambapo amesema kuwa chanzo kikubwa cha ajali.
Amesema kuwa madereva ndio wamekuwa chanzo kikubwa cha ajali kwa kutofuata sheria za barabarani, jambo ambalo limekuwa likisumbua kwa muda mrefu.
“Niwaase sana madereva wa Arusha mliopata elimu hii ya usalama barabarani, mkawaelimishe na hao wengine ambao hawajajumuika, waje nao kupata elimu hii,”amesema DC Daqaro