Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Hashim Mgandilwa amezindua mtambo wa kukabiliana na maafa ambayo yamekuwa yakijitokeza mara kwa mara na kuikumba jamii.
Uzinduzi huo umefanyika Temeke jijini Dar es salaam, ambapo mradi huo unategemewa kuwa msaada mkubwa katika kusaidia jamii wakati wa majanga kama mafuriko, maporomoko ya udongo kwenye baadhi ya machimbo pia majanga ya moto.
Akimuwakilisha mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Mgandilwa amesema kuwa mpango huo umeandaliwa kwaajili ya kukabiliana majanga ndani ya mkoa wa Dar es salaam hivyo utakuwa ni mfano wa kuigwa.
“Leo hii tupo hapa kukabidhi na kuzindua mpango huu, ni lazima wahusika wawe tayari hata kama ukipigiwa simu usiku, kwa sababu huu ni wajibu wenu,”amesema Mgandilwa