Waziri wa Katiba na Sheria amempongeza na kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli kwa kuunda kamati ya uchunguzi wa mikaba ya biashara ya dhahabu na makinikia ambayo yalikuwa yakisafirishwa nje ya nchi.

Ameyasema hayo Ikulu jijini Dar es salaam wakati wa kukabidhi ripoti ya mazungumzo kati ya watalaamu wa Serikali na Kampuni ya Barrick Gold Mine kuhusu makubaliano yaliyofikiwa katika marekebisho ya mikataba ya biashara ya madini aina ya dhahabu.

Amesema kuwa mazungumzo hayakuwa rahisi lakini anashukuru wameweza kufikia makubaliano ambayo yataweza kuinufaisha nchi katika kuleta maendeleo katika jamii ya Watanzania.

“Kwanza nikushukuru na kukupongeza kwa kuunda kamati mbalimbali ili kufanya uchunguzi, kwani tumeweza kufanya mazungumzo ambayo yameweza kufanikiwa kwa kiasi kikubwa,”amesema Prof. Kabudi

Video: DC Mgandilwa azindua mtambo wa dharula wa kukabiliana na maafa
Nchemba awataka wananchi kushirikiana