Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema amekutana na wadau mbalimbali wa maji jijini Dar es salaam kujadili changamoto zinazowakabili wananchi na kuona jinsi gani wanavyoweza kukabiliana nazo.
Amesema kuwa changamoto zinazolikabili jiji la Dar es salaam zinaweza kutatuliwa na wadau kwa kushirikiana na wananchi ili kuweza kuondokana na uharibifu wa vyanzo vya maji na upatikanaji wa maji safi.
Hata hivyo, amesema kuwa changamoto kubwa inayoikabili sekta ya maji jijini Dar es salaam ni utandazaji wa mabomba ambayo siku zote umekuwa ni mgumu ingawa maji yanazlishwa kwa wingi.