Mwenyekiti  wa Bodi ya Maendeleo na Ushirika Nchini Dkt. Titus Kamani ametoa anyo kali kwa viongozi wa vyama vya ushirika nchini kuacha tabia ya kufuja mali za wanachama ili wao waweze kunufaika na si ushirika kama ilivyokuwa imekusudiwa na ushirika huo.

Ametoa onyo hilo mkoani Simiyu alipokuwa akizungumza na Dar24 Media ambapo amesema kuwa viongozi wa vyama vya ushirika wamekuwa ni chanzo cha vyama vingi vya ushirika kuteteleka.

Aidha, ameongeza kuwa kiongozi yeyote yule wa ushirika mwenye nia mbaya na chama chochote cha ushirika ni bora akajiengua mapema.

“Serikali imekusudia kurejesha heshima ya ushirika nchini kwa lengo la kuwasaidia wakulima ili waweze kujikwamua kwenye umasini wa miaka mingi uliokuwa ukisababishwa na baadhi ya watu ambao sio waaminifu kwa kuwarubuni wakulima katika mazao yao,” Amesema Dkt. Kamani.

 

Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Septemba 7, 2018
Tetesi za Kim Kardashian kutoka na Drake zapashwa moto