Jiji la Tanga ni miongoni mwa majiji yenye maajabu ya ustaarabu wa pekee na mpangilio utakaokufanya utamani kuendelea kubaki na kudekezwa na hali ya jiji hilo.
Kutokana na upekee wa mpangilio wa barabara zake 21 zinazofuatana pamoja na utamaduni wake, Dar24 ilipiga kambi jijini humo na kuzungumza na wenyeji wa jiji hilo linalotambulika pia kwa ‘raha na mahaba’.
Angalia video hii kuona makala fupi iliyobeba majibu ya siri ya mpangilio wa barabara zake, utamaduni wa ustaarabu wa maneno na mavazi utaowavuta wageni.
‘Tanga waja leo kuondoka majaaliwa’.