Mwenyekiti wa Bodi ya NHIF, Anne Makinda amesema kuwa kila mtanzania anatakiwa kuwa na bima ya afya ili kuwa na uhakika wa matibabu na kuweza kutimiza majukumu yake ya kila siku na kuepukana na umaskini.

Ameyasema hayo mapema hii leo mjini Dodoma mara baada ya kutembelea  maonyesho ya Nane Nane ambapo amesema kuwa katika zama hizi wananchi wanatakiwa kuchapa kazi kama Rais Dkt. Magufuli anavyotuhimiza,

“Ili tuweze kuendana na kasi hii hatuna budi kuwa na uhakika na afya zetu na Serikali imetuletea utaratibu huu wa bima ya afya ambao ni rahisi kwa kila mtu kujiunga na kuwa na uhakika wa matibabu pindi anapougua,”amesema Makinda

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Bernard Konga amesema kuwa amejipanga kutoka na kwenda kuwafuata watu walipo ili kuweza kuwasajili na huduma za Mfuko huo.

Aidha, ameongeza kuwa kwa sasa Mfuko unafanya kampeni ya uhamasishaji wa huduma ya bima ya afya kwa watoto walio chini ya miaka 18 ijulikanayo kama TOTO AFYA KADI.

Naye Meneja wa NHIF Mkoani Dodoma, Salome Manyama amesema wazazi na walezi wamepata mwitikio na kufika kusajili watoto wao katika huduma ya TOTO AFYA KADI katika maonyesho hayo.

Magazeti ya Tanzania leo Agosti 9, 2017
Video: Fahamu ustaarabu wa kustaajabisha Tanga na siri ya barabara 21