Maisha ya mwanadamu kwa kiwango kikubwa yanategemea Choo, Moja kati ya taifa linalosemwa sana kwa matumizi ya choo ni India ambapo asilimia 70 ya watu wanaoishi vijini nchini humo hawatumii vyoo badala yake hujisaidia porini, au pembezoni mwa barabara hali iliyopelekea ipitishwe kwamba ukitaka kuoa ni lazima kumjengea mkwe choo kama sehemu ya mahali.
Tanzania kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa mwaka 2017 na Wizara ya Afya zimeonesha kwamba kuna tatizo la choo bora ambapo kwa takribani asilimia 40 ya watanzania hawana vyoo bora yaani takwimu hizo zinaonesha kwamba katika kila kaya 10, kaya nne hazina vyoo bora.
Kupitia Wizara ya Afya Tanzania imetoa ufafanuzi na kutofautisha kati ya choo bora na choo cha kisasa kwa kuangalia uwezo wa mtu kiuchumi ambapo imesema;
Choo Bora ni kile ambacho kina kuta nne imara, paa imara, mlango mzuri, sakafu inayosafishika, kiwe na bomba la kupumua, kiwe na maji na sabuni ya kunawa mikono baada ya kujisaidia.
Aidha, Balozi wa Choo, Mrisho Mpoto amesema kuwa sio kwamba watu hawana hela ya kujenga choo bora, ila watu wanachukilia poa choo, ametoa hamasa kwa watanzania kujitahidi kuzingatia choo bora kwani magonjwa mengi yakuambukiza chanzo chake ni uchafu.
Mjadala juu ya choo bora uliibuliwa maeneo ya Kiwalani jijini Dar es salaam katika kipindi cha On The Bench kinachofanywa na chombo cha habari mtandaoni, Dar24 ambapo kipindi hiko kinawakusanya pamoja wadau mbalimbali viongozi, watunga sheria wataalam wa mambo mbalimbali kujadili mambo yanayoigusa jamii.
Sikiliza hapa Kaimu Afisa Afya Kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, Regnald Mlaya, Balozi wa nyumba ni choo, Mrisho Mpoto, pamoja na wanachi wa Kiwalani wakifafanua zaidi.
Sikiliza hapa mwanzo mwisho.