Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi, Katibu Mkuu wa TFF, Mwesigwa Selestine na Mhasibu wa Shirikisho hilo, Nsiande Mwanga wamefikishwa Mahakamani leo Julai 3, 2017 wakikabiliwa na mashitaka 28, ikiwemo ya utakatishaji fedha.
Hata hivyo watuhumiwa hao wataendelea kusota rumande baada ya upande wa Jamhuri kushindwa kukamilisha upelelezi wa kesi inayowakabili watuhumiwa hao, ambapo Mahakama ya Hakimu Mazi Kisutu imetupilia mbali maombi ya upande wa utetezi kutaka, Malinzi na wenzake kupatiwa dhamana.
Kutokana na kukataliwa maombi hayo kesi ya Malinzi na wenzake iliahirishwa hadi July 17, 2017.
Aidha, Mahakama hiyo imewaonya Mawakili wa upande wa utetezi ikiwataka waache ubabaishaji wa kuizungumzia kesi hiyo kwenye vyombo vya habari badala yake wawasilishe hoja zao mbele ya Mahakama.