Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amesema kuwa hakuna kiongozi yeyote mwenye mamlaka ya kuingiza mizigo kutoka nje ya nchi bila kulipia kodi.
Ameyasema hayo hii leo wilayani Chato mkoani Geita alipokuwa akizungumza wa madiwani, ambapo amesema kuwa mzigo wowote unaopitishwa bandarini ni lazima ulipiwe kodi.
Amesema kuwa ni vyema viongozi wakajenga tabia ya kuwatumikia wananchi na si vingine ambayo wamekuwa wakifanya.
“Kuna sakata la huyu mkuu wa mkoa wa Dar es salaam ameleta makontena ya vifaa vya walimu, eti anasema kachangiwa na Watanzania waliopo nje nchi, ni lazima yalipiwe kodi,”amesema JPM