Jeshi la Wananchi wa Tanzania JWTZ limesema kuwa hivi karibuni limepokea taarifa kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kuhusu kusudio la kuwasitishia huduma ya umeme Machi 27, 2017 kutokana na deni kubwa.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Venance Mabeyo wakati akizungumza na Waandishi wa habari leo Machi 26, 2017 ambapo amethibitisha kuwa JWTZ inadaiwa na TANESCO zaidi ya shilingi Bilioni 3.
Amesema kufuatia madai hayo ya TANESCO, jeshi hilo litahakikisha kesho linalipa kiasi cha shilingi Bilioni 1 ili kuonyesha nia njema ya kutaka kulipa deni hilo ili lisikatiwe umeme. Bofya hapa kutazama.