Msanii wa Bongofleva Nay wa Mitego amekamatwa na Jeshi la Polisi Morogoro.

Akithibitisha kukamatwa kwa Msanii huyo, Kamanda wa Polisi Morogoro Ulrich Mtei amesema kwamba nikweli Nay wa Mitego anashikiliwa Morogoro na shauri lake sio la Morogoro, Polisi Morogoro wamepata tu maelekezo kwamba atafutwe na kukamatwa kwani alikuwa akitoroka na huhuma zake zipo Dar es salaam.

Kamanda Mtei amesema Nay wa Mitego alikuwa akitoroka, hivyo baada ya taarifa kuwa anatafutwa ndipo Jeshi hilo likamkamata na anatakiwa kusafirishwa kwani shauri lake lipo Kituo cha Polisi cha Kati Dar es salaam.

“Ni kweli huyu Bwana anashikiliwa Morogoro na shauri lake sio la Morogoro…, tulipata tu maelekezo kwamba tumtafute“ amesema Kamanda Mtei.

Nay wa Mitego amekamatwa na Polisi Morogoro jana usiku ambapo Jeshi hilo halikueleza moja kwa moja sababu za kukamatwa kwa msanii huyo kutokana na utaratibu wa wa Jeshi hilo, hivyo taarifa kamili ya kukamatwa kwa msanii huyo itatolewa na Polisi Dar es salaam.

Video: JWTZ wazungumza kuhusu deni TANESCO
Ziwa Jipe hatarini kutoweka, Bwawa la Nyumba ya Mungu latajwa pia