Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa amesema uamuzi wa kampuni ya Kichina kujenga kiwanda kikubwa cha saruji mkoani Tanga ni wa faraja kutokana na mahitaji makubwa yaliyopo nchini.
Majaliwa amesema hayo wakati akizungumza na ujumbe wa kampuni ya Sinoma na kampuni ya Hengya Cement (T) Ltd ambao ulimtembelea ili kumpa taarifa ya uamuzi wao huo. Ujumbe huo ulifuatana na Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martin Shigella na viongozi kutoka TIC na Wizara ya Viwanda na Biashara.
“Wawekezaji wa sasa wako tayari kwenda na teknolojia ya kisasa kwa hiyo Watanzania wawe tayari kuwapokea wawekezaji ili tushirikiane nao kukuza uchumi wetu na Tanzania itoke hapa ilipo na kwenda kwenye uchumi wa kati,” amesema Waziri Mkuu.