Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimeitaka Serikali kuifuta adhabu ya kifo ambayo inakwenda kinyume na haki za binadamu.

Hayo yamesemwa hii leo jijini Dar es salaam na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC, Ana Henga, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, ambapo amesema kuwa adhabu ya kifo inaondoa uwezekano wa mkosaji kujirekebisha na badala yake ni kuendeleza ukatili na kuondoa ubinadamu.

Amesema kuwa Tanzania inapaswa kujifunza kutoka kwa mataifa mengine duniani ambayo hayatekelezi adhabu ya kifo na badala yake kutoa adhabu mbadala kama vile kifungo cha maisha na kazi ngumu kwa watuhumiwa wa mauaji ili kulinda haki ya msingi ya kuishi.

Aidha, Henga amesema harakati za kupinga adhabu ya kifo hazimaanishi kuwa ni kutetea uhalifu, hasa mauaji ila ukweli ni kwamba, hakuna ushahidi kuwa uwepo wa adhabu hiyo unaweza kupunguza uhalifu badala yake umekuwa ukiongezeka.

Hata hivyo, ameongeza kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi chache duniani kama vile China, Korea Kaskazini na Marekani ambazo zinaruhusu na kutekeleza adhabu ya kifo katika sheria zake.

Kocha Toto Africans azuiwa kukaa kwenye benchi
Uchaguzi bodi ya ligi jumapili hii