Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika(TLS), awametaka wanachama wote wa TLS nchi nzima kususia kuhudhuria mahakamani kufanya kazi za uwakili na kwenye mabaraza kwa siku mbili Jummanne na Jumatano ili kupinga shambulio dhidi ya ofisi za IMMMA Advocates
Ameyasema hayo hii leo jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, ambapo amesema kuwa kufanya hivyo ni ishara ya kupinga tukio hilo ambalo amesema sio la bahati mbaya na huenda linahusika na kazi za Mawakili wa IMMMA ambao wanafanya kazi na Kampuni ya Acacia yenye mgogoro na serikali
Amesema kuwa wamepokea kwa masikitiko kushambuliwa kwa ofisi za IMMMA zilizokpo jijini Dar es salaam usiku wa kuamkia jana baada ya kuteketea kwa moto hivyo amewataka wanachama wote wa TLS kugoma kuhudhuria mahakamani
“Baada ya kukaa kikao cha Baraza la uongozi la TLS kilichofanyika jana tarehe 26/08/2017 kujadili shambulio la mabomu. Baraza limepata taarifa kuwa kuna kikundi cha watu kadhaa kikiwa kimevalia sare za jeshi la polisi na wakiwa na silaha za moto kiliwateka nyara walinzi binafsi wa IMMMA advocates na kuingia ndani na kutega milipuko na madumu manne ya mafuta ya petroli katika jengo zilizopo ofisi hizo,”amesema Tundu Lissu
-
Sheikh Salum ataka waliokwamisha mahujaji uwanja wa ndege wakamatwe
Hata hivyo, ameongeza kuwa muda mfupi baadae, milipuko hiyo ililipuka na kusababisha uharibifu mkubwa katika jengo hilo na majengo jirani, kwa sababu ilikuwa usiku, hakuna mtu yeyote alieumia au kupoteza maisha kutokana na shambulio hilo.