Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa amewaagiza viongozi wa ngazi mbalimbali kuweka utaratibu utakaoruhusu huduma za afya kuendelea kutolewa kwa wananchi katika maeneo yao hata kama zoezi la usafi la kila mwezi litakuwa linaendelea.
Majaliwa ametoa agizo hilo leo Mei 11, 2017 Bungeni mjini Dodoma katika kipindi cha maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu wakati akijibu swali la Mheshimiwa Abdallah Ulega mbunge wa Mkuranga.
Amesema kuwa Serikali imeweka utaratibu wa wananchi kushiriki katika shughuli za usafi wa mazingira siku ya Jumamosi ya mwisho wa mwezi, zoezi ambalo linashirikisha watu wote wakiwemo wafanyabiashara na watoa huduma nyingine zoezi linalofanyika kuanzia saa 12.00 asubuhi hadi saa 4.00 asubuhi.