Serikali imetoa tamko la kupiga marufuku uuzwaji na usambazaji wa pombe kali aina ya viroba pamoja na matumizi ya vifungashio vya plastiki vinavyotumika katika biashara ya uuzaji wa pombe kali nchini kuanzia tarehe 01.03.2017
Hayo yamesemwa mapema hii leo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, January Makamba alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu tamko lililotolewa na Serikali la utaratibu wa usitishwaji wa uuzaji wa pombe aina ya virob.
Makamba amesema kuwa utekelezaji wa katazo hilo utazingatia ibara ya 8(1) na 14 pia sheria ya mazingira ya mwaka 2004 na kanuni zake zilizotungwa kupitia kifungu cha 230 ibara ya(2)(f)cha sheria hiyo na sheria ya leseni za vileo namba 28 ya mwaka 1968 pamoja na marekebisho yake ya mwaka 2012.
Hata hivyo, amesema kuwa utekelezaji wa agizo hilo utaanza kuanzia siku ya kesho katika mikoa yote ya tanzania bara na operesheni ya ukaguzi pamoja na utekelezaji wa agizo hilo la Serikali utaendeshwa katika kila mkoa kuanzia tarehe 02.02.2017 kwa kupitia kamati za ulinzi na usalama pamoja na kamati za mazingira katika ngazi ya mkoa ,wilaya,tarafa,kata,vijiji na mtaa.