Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ametoa wito kwa Wizara ya Elimu, Jeshi la Polisi na Wazazi kulinda Sheria za Usalama barabarani ili kulinda maisha na ndoto za watoto.

Ameyasema hayo katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha wakati wa kuaga miili ya wanafunzi 33, walimu wawili na dereva wa Shule ya Msingi Lucky Vicent waliofariki kwa ajali ya gari Mei 6 mwaka huu Mkoani Arusha.

“Msiba huu umemgusa kila Mtanzania, hivyo tuzidi kuwaombea Mungu azilaze roho za marehemu mahali pema peponi, hivyo tujipe moyo na nguvu kwamba hili limetokea na kwa Mwenyezi Mungu tujirudishe” amesema Makamu wa Rais.

Kwa upande wake Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Prof. Joyce Ndalichako ametoa pole kwa wazazi wote walio ondokewa na watoto na ndugu zao, wafiwa na watanzania wote walioguswa na msiba huo.

Naye Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Abdulrahman Kinana amewapa pole wazazi na wanajumuiya wote na kusema kuwa kama kuna kitu kinatuunganisha sote ni kifo kwani kila binadamu ana mwisho wake

Tanzania ni nchi pekee barani Afrika kuwa na taasisi ya kudhibiti kemikali
Wadau wa madini waiomba Serikali kutoa elimu ya uchimbaji madini