Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ameahidi kutatua changamoto zinazowakabili mabahari kwa lengo la kuwawezesha kupata kazi ndani na nje ya nchi.

Ameyasema hayo jijini Dar es salaam wakati wa ufunguzi wa mkutano wa mabaharia, ambapo amesema atashughulikia changamoto zinazowakabili na kuzitafutia ufumbuzi ili ziweze kutengeneza fursa ya watu kupata kazi, kuheshimika na usalama wa mwajiriwa, uhakika wa kazi pamoja na kufanya kazi kwa ufanisi.

“Naamini changamoto zote hizi ambazo nimeziona zipo kwenye makundi matatu ninaweza kuzitatua na tutaendelea kushirikiana na kuweka mikakati itayowawezesha mabaharia kunufaika, na niwahakikishie kwamba tutafanikiwa.”amesema Makonda.

Aidha, amebainisha kuwa zikitokea nafasi za kazi kwa mabaharia watapewa kipaumbele ili waweze kulinda vyema rasilimali za nchi na kuepusha kusafirisha Mali za magendo na kusaidia kukuza uchumi wa taifa kwa kuweza kulipa kodi kikamilifu

 

Magazeti ya Tanzania leo Novemba 16, 2017
Donge nono la mil. 10 lamuibua kigogo Takukuru