Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amesema kuwa ametafuta njia mbadala kwa wale wanaopanda bodaboda bila kuvaa kofia ngumu (Helmenti) kwa kudai kukwepa magonjwa katika kofia hizo.
Makonda amesema hayo leo januari 26, 2017 jijini Dar es salaam wakati akiongea na waandishi wa habari ambapo ameeleza kuwa suala la abiria na waendesha bodaboda kukwepa kuvaa helmenti limekuwa likitolewa elimu kwa wananchi kuwa ni hatari kwa maisha yao kwani wengi wamepata madhara makubwa kutokana na uzembe huo wanapopanda bodaboda.
Amesema kutokana na sababu zinazotolea na baadhi ya wananchi wakidai kupata magonjwa katika helmenti hizo, tayari amesha agiza helmenti za kutosha pamoja helmenti maalum za ‘takewaway’ na abiria atapewa ikiwa mpya hivyo atavaa mwisho wa safari ataamua kuitunza au kutupa.