Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda, leo ametaja orodha ya majina 65 ya watuhumiwa wengine wanaojihusisha na biashara ya madawa ya kulevya huku wakiwemo watu maarufu kama Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga, Yusuf Manji, Mbowe mbunge wa Hai, Hussen Pambakali, Mchungaji Josephat Gwajima, ambao wanatakiwa kuripoti kituo cha Polisi cha Kati siku ya Ijumaa kwa ajili ya mahojiano.
Makonda ametaja orodha ya majina 65 wanaotakiwa kufika kituoni hapo kwa ajili ya mahojiano katika kampeni yake ya kupambana na biashara haramu ya madawa ya kulevya.
Ameyasema hayo mapema hii leo Februari 8, 2017 ofisini kwake Jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.