Serikali imesema kuwa iko tayari kufanya kazi na makampuni ya matangazo ya biashara nchini endapo yataunda umoja na ushirikiano.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Jenista Mhagama katika uzinduzi wa ushirika wa makampuni ya biashara.
“Mara nyingi tumeshindwa kutumia fursa nyingi zilizopo kwa ajili tu ya kukosa mshikamano, lakini kwa hiki mlichokifanya kwasasa mtapiga hatua kubwa,”amesema Mhagama
Hata hivyo, ameongeza kuwa hapo awali hapakuwa na mshikamano baina ya makampuni yanayofanya biashara, hivyo kupelekea makampuni hayo kukosa fursa nyingi.