Waziri Mkuu Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Fredrick Sumaye amesema kuwa kunyang’anywa kwa shamba lake la Mabwepande ni muendelezo wa mkakati wa serikali wa kumtaifisha mashamba hayo ambayo ni mali yake.
Ameyasema hayo hii leo jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, ambapo amesema kuwa tangu enzi za uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 baada ya kuhamia chadema baadhi ya viongozi walisema dawa yake ni kumnyang’anya mashamba yake yote ili afilisike.
Amesema kuwa baraka za wavamizi waliovamia mashamba yake zimetoka kwa viongozi wa ngazi za juu yenye lengo la kulipiza visasi vya kisiasa kwa kuwa Serikali ilishasema mapema kuwa itafanya hivyo.
“Shamba langu limetwaliwa na Rais, na kugawiwa kwa wananchi kwa kisingizio cha kwamba halijaendelezwa lakini kitu ambacho si kweli kwani tulizuiwa kuliendeleza, hivyo hatukuwa na namna ya kufanya,”amesema Sumaye
-
Tanesco kuwashughulikia wafanyakazi wahujumu
-
Kizimbani kwa kula nyama za binadamu
-
Kikwete: Wanaosubiri kustaafu ndipo waanze kilimo, ufugaji wamechelewa
Hata hivyo, ameongeza kuwa Serikali imedhamiria kulipa visasi vya kisiasa vyenye dhamira moja tu ya kutaka kumtaifisha mali zake hasa mashamba yake ya Mabwepande.