Shirika la umeme Tanzania (Tanesco)limesema kuwa litachukua hatua kali dhidi ya wafanyakazi wake ambao wamekuwa wakilihujumu ikiwamo kuwafukuza kazi.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani katika uzinduzi wa mradi wa  awamu ya tatu wa usambazaji umeme vijijini REA uliofanyika katika kijiji cha Kirya Wilayani Mwanga mkoani Kilimanjaro.

“Watumishi wote wa umma waliozoea kucheza dili chafu na vishoka na kuhujumu miradi ya umeme wakati wa kuwaunganishia wananchi umeme dawa yao imeiva, tutawafukuza kazi wale wote watakaobainika kufanya uhujumu,”amesema Kalemani

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Wakala wa Nishati Vijijini, Mhandisi Gissima Nyamo amesema kuwa awamu ya tatu ya mradi huo katika mkoa wa Kilimanjaro utagharimu kiasi cha shilingi bilioni 16 na utatekelezwa kwa muda wa miezi 24.

Jay Moe na Madee watoa somo kwa nyimbo zinazotoka hivi sasa
Nandy: Ruge alivunja CD ya nyimbo zangu